
Wasifu wa Mndee ni riwaya ya kusisimua inayohusu masaibu yanayowakuta watoto wa kike. Masaibu haya ni pamoja na kudanganywa au kulaghaiwa kimapenzi na hatima yake inajulikana: mimba za utoto na kusalitiwa (kukataliwa). Riwaya hii haizungumzii tu masaibu haya yawapatao wasichana na kuyaachia hapohapo - lahasha! Riwaya hii inatoa pendekezo na mbinu ambazo watoto wa kike wanaweza kuzitumia ili kuepukana na masahibu kama hayo. Vilevile inatoa mwelekeo wa nini cha kufanya baada ya masahibu kumkuta mtoto wa kike. Miongoni mwa masuluhisho hayo ni kuendelea na masomo baada ya kujifungua na kujipatia maisha yako kama watu wengine. Kwa hakika riwaya hii inatoa mwangaza kwa wasichana au wanawake waliokata tamaa baada ya kusalitiwa kimapenzi. Je ni mwangaza gani huo? Soma riwaya hii ujifunze na uchukue hatua.
Details
- Publication Date
- Mar 20, 2013
- Language
- Swahili
- ISBN
- 9781300854845
- Category
- Fiction
- Copyright
- All Rights Reserved - Standard Copyright License
- Contributors
- By (author): elizabeth mahenge
Specifications
- Pages
- 70
- Binding Type
- Paperback Perfect Bound
- Interior Color
- Black & White
- Dimensions
- US Letter (8.5 x 11 in / 216 x 279 mm)