Kazi aliyokuwa ametumwa Arusha ilimfanya Mpelelezi hatari na makini Jacob Matata ahisi kuwa ilikuwa ni safari ya hatari, lakini hakudhani kuwa ingekuwa ni hatari kiasi hicho. Alipoweka tu mguu wake katika jiji hilo alipokelewa na harufu ya tofauti, si ile ya ubaridi wa Arusha, bali ya Mauti. Hivyo kila hatua aliyokuwa akijaribu kupiga ilizidi kumsogeza jirani zaidi na kifo. Mbaya zaidi ni pale alipoambiwa kuwa ZAMU YAKE YA KUFA ilikuwa imefika. Hapo ndipo ilimbidi kupambana na genge la kutisha na lililosheheni sumu ya mauti. Jacob Matata alipigania kila tone la hewa aliyokuwa akiivuta katika mji wa Arusha.
Hali ya ujanja, utaalamu wa kupigana na utumiaji wa silaha wa hali ya juu inatawala huku pande zote zikihitaji ushindi.
Ukisoma riwaya hii utajua kuwa, kuna mtu mwenye kipaji cha kutumia kalamu, meza na karatasi katika kuwapa wapenzi wa riwaya kile nafsi zao zinataka. Riwaya nyingine za Japhet S. Nyang’oro ni kama MKONO WA SHETANI, BEI HALALI NI KIFO CHAKO na HARUFU YA MAUTI. Zitafute!
Details
- Publication Date
- Aug 9, 2007
- Language
- Swahili
- Category
- Fiction
- Copyright
- All Rights Reserved - Standard Copyright License
- Contributors
- By (author): Japhet Nyang'oro
Specifications
- Pages
- 111
- Binding Type
- Paperback Perfect Bound
- Interior Color
- Black & White
- Dimensions
- Pocket Book (4.25 x 6.875 in / 108 x 175 mm)